Hesperian Health Guides
Huduma ya ganzi
HealthWiki > Toleo Jipya: Mahali Pasipo na Daktari > Maumivu tumboni, kuhara, na minyoo > Huduma ya ganzi
Lidokeini (Lidocaine), Lignokeini (Lignocaine)
Lidokeini (Lidocaine) ni dawa ya ganzi ambayo inaweza kuchomwa eneo linalozunguka kidonda kuachia ganzi ili mtu asisikie maumivu. Hii ni muhimu kabla ya kukamua jipu au kushona kidonda. Kama utaamua kuondoa damu iliyoganda kutoka kwenye bawasiri, tumia lidokeini kwanza.
Choma sehemu mbili-ndani na chini ya ngozi inayozunguka eneo ambalo unakwenda kukata au kushona, ukiacha sentimeta 1 katikati. Kwanza, safisha ngozi vizuri, halafu choma sindano hiyo ya lidokeini. Tumia wastani mililita 1 ya dawa ya ganzi kwa kila sentimita 2 za ngozi. (Usitumie zaidi ya mililita 20 kwa pamoja.)
Angalia Dawa, vipimo, na matibabu (inaandaliwa) kuhusu jinsi ya kutoa huduma ya sindano kwa usalama.