Hesperian Health Guides
Dawa zingine za kutibu kuhara
HealthWiki > Toleo Jipya: Mahali Pasipo na Daktari > Maumivu tumboni, kuhara, na minyoo > Dawa zingine za kutibu kuhara
Furoti Diloksanaidi (Diloxanide furoate)
Diloksanaidi (Diloxanide) hutumika pamoja na antibiotiki kutibu ameba. Kama huwezi kupata dawa hii, jaribu paromomaisini (paromomycin) au iodokino (iodoquinol) badala yake.
Kwa nadra dawa hii husababisha gesi tumboni, maumivu tumboni, au kichefuchefu. Tumia na chakula.
Usitumie diloksanaidi (diloxanide) ndani ya miezi 3 ya kwanza ya ujauzito. Epuka dawa hii wakati unapokuwa unanyonyesha.
Baada ya kumaliza dozi ya metronidazo au tiba nyingine ya ameba, anza kutumia diklosanaidi (diloxanide).
Chini ya miaka 3: toa miligramu 62 (⅛ ya kidonge cha miligramu 500), mara 3 kila siku kwa siku 10.
Miaka 3 hadi 7: toa miligramu 125, mara 3 kila siku kwa siku 10.
Miaka 8 hadi 12: toa miligramu 250, mara 3 kila siku kwa siku 10.
Zaidi ya miaka 12: toa miligramu 500, mara 3 kila siku kwa siku 10.
Kwinakrini (Quinacrine)
Dawa ya Kwinakrini (Quinacrine) hufanya kazi vizuri katika kutibu giardia, lakini huwafanya watu kujisikia vibaya zaidi. Hutumika kwa sababu siyo ghali sana.
Maumivu ya kichwa, kizunguzungu, na kutapika ni madhara ya kawaida.
Zaidi ya miaka 10: toa miligramu 100, mara 3 kila siku kwa wiki 1.
Zinki
Zinki husaidia watu wanaoharisha kupata nafuu haraka. Inapaswa kutolewa pamoja na kinywaji cha kuuongezea mwili maji.
Kwa watoto wachanga, vidonge vinaweza kusagwa na kuchanganywa na maziwa ya mama au maji kidogo. Unaweza kupata kidonge ambacho huyeyuka haraka kwenye maji au kimiminika kingine.
Zaidi ya miezi 6: toa miligramu 20, mara moja kila siku kwa siku 10 hadi 14.